Hadithi za kusisimua

IJUE HISTORIA HALISI NA MAAJABU YA BERMUDA TRIANGLE.
           Bermuda Triangle ni eneo la pembe tatu la bahari lililopo kati ya nchi tatu katika bahari ya Atlantiki.Miji hiyo ni Bermuda,Puerto Rico na Fort Lauderdale.Meli,watu na ndege mbalimbali zimeripotiwa kupotea kutokuonekana milele katika eneo la Bermuda Triangle.Muda mfupi eneo hili limekuwa likipata umaarufu na kupewa jina la Devil's sea (Bahari ya Shetani) ambapo binadamu wamekuwa wakiamini au kujenga imani potofu za kishirikina kuwa shetani amekuwa na makazi katika eneo hilo na kuwapoteza wasafiri wa majini ikiwa ni pamoja na vyombo vyao vya usafiri,lakini uhalisia katika eno hili la maji mafupi ni ukweli kuhusu shetani? au Aliens wamekuwa wakitumia eneo hili kama kituo chao katika dunia.Inawezekana kuna ukweli juu ya swala la kina hiki kuwameza watu katika eneo hili.
           Historia ya eneo hili imekuja kuzuka katika chombo cha habari cha Associated Press dispatch cha Septemba 16,1950.Mwana habari E.V.M Jones aliandika kuhusu upoteaji wa ajabu wa meli na ndege  katikati ya pwani ya Florida na Bermuda.Miaka miwili baadae kipengele kilionekana katika jarida ikiwa na kipengele kingine kilicho andikwa na George X. Sand kuhusu "Mtiririko wa kutisha wa upoteaji wa vyombo vya majini" ambao umechukua nafasi katika miaka kadhaa iliyopita.
           Ulipita muda mrefu kabla ya mawazo na mitazamo iliyotolewakuhusu kipande hiki cha bahari. M.K Jessup aliandika kuhusu upoteaji na akatoa mawazo kuhusu upeo mkubwa wa kiakili wa Aliens ( Viumbe wa Ajabu ) kuhusiana na swala hili katika kitabu cha "The Case for the UFO". Urejeo wa kitabu hicho ulikuja kutolewa na Donald E. Kyhoe wa kitabu cha "The Flying Saucer Conspiracy" cha 1955.Frank Edwards wa "Stranger Than Science" alikuja kukubaliana na wazokuhusu Aliens kwa kuwa na makazi katika eneo hilo la pembe tatu pia.Mwishoni Vincent H. Gaddis alikuja na ripoti kuhusu "Bermuda Tringle".Huyu aliandika kipengele katikamwezi wa Februari ya mwaka 1964 ambapo baadae alikuja kuandika historia katika kitabu chake "Ivisible Horizons" iliyoitwa "The Deadly Bermuda Triangle".
            Mika mingi imepita  na vipengele,vitabu,mtiririko wa vipindi vya televisheni na filamu mbalimbali zimetengenezwa kuhusu kitu hiki cha kushangaza,lakini mtu yeyote mwenye mawazo juu ya swala hili lazima atajiuliza juu ya kwanini meli,ndege na watu wamekuwa wakipotelea katika kipande hiki cha bahari? Je,hawaogopi kusafiri? 
            Moja ya historia maarufu katika eneo la Bermuda Triangle juu ya kupotea kwa kushangaza ni ya ndege ya Air Flight 19.Je,nini kilitokea?
            Desemba 5 ya mwaka 1945,ndege ya mabomu iliondoka katika kituo cha kijeshi cha ndege katika ngome ya Lauderdale na hawakurudi.Ndege hii ilikuwa na watu 14 ambao 13 miongoni mwao walikuwa ni wanafunzi wa urubani katika hatua ya mwisho ya mafunzo wakiwa na Luteni Charles Taylor.Marubani wengine watano walikuwa tayari wamekwisha kusafirishwa kutoka katika kituo cha Miami cha ndege.Luteni Taylor alikuwa tayari na uelewa mzuri wa eneo la Florida ingawa hakuwa na uelewa wa kusafiri angani katika eneo la Bahamas ambapo ndio ndege ya Flight 19 ilitakiwa kuelekea.
            Wazo lao kwa siku ile ilkuwa ni mazoezi ya kulipua mabomu katika eneo la kufugia kuku maili 56 kutoka katika kituo cha kijeshi cha ndege katika ngome ya Lauderdale.Swala hilo kwa mara moja lilifanikiwa.Marubani hao walitakiwa kundelea kuelekea upande wa mashariki kwa maili 67 na baadae kuelekea kaskazini kwa maili 73.Baadae walitakiwa kurudi kusini magharibi kuelekea nyumbani yaani katika eneo waliloanzia safari.Kwa maneno mengine walikuwa wakisafiri safari ya njia ya pembe tatu ambayo iliitwa Bermuda Tringle.
             Muda wa saa 9:50 mchana,rubani na waelekezaji wa ndege ile,Luteni Robert Cox walikuwa karibu kutua katika ngome ya Lauderdale.Walisikia sauti ya mtu aliyeitwa Powers kupitia mawimbi ya redio.Powers akajibu "Sijui hapa tulipo ni wapi ,lazima tutakuwa tumepotea baada ya kugeuka kwa mara ya mwisho".
             Baada ya muda mfupi ,Luteni Cox aliweza kugundua sauti kupitia mawasiliano ya radio na rubani mwingine wa wasafiri waliopotea katika bahari wakiongea na Luteni Taylor.Alitaarifiwa kuwa dira za Taylor zilikuwa hazifanyi kazi tena na hivyo walikuwa na uhakika kuwa walikuwa katika eneo la karibu,yaani la Florida,ingawa hakujua jinsi ya kufika katika eneo au ngome ya Lauderdale.
             Tangu hapo mawasiliano yakawa yamekatika kati ya kituo cha Lauderdale na ndege ya wanafunzi wa urubani ya Flight 19.Hii ilichangiwa na hali ya hewa ya anga yaani Atmospheric Condition kwa lugha ya kitaalamu ambayo ilichangia katika ukatikaji wa mawasiliano ya mawimbi ya radio.Mpaka kufikia muda wa saa 11:15 ya jioni,ndege ya Taylor ilikuwa bado haijatua katika kiwanja changome ya Lauderdale.
             Baada ya kuona mawasiliano yamekosekana,Luteni Taylor aliamua kuendelea na mafunzo na wanafunzi wake kuelekea kaskazini.Ndege ya uokoaji iltumwa muda wa saa 12:20 jioni.Ilikuwa ni ndege yenye uwezo wa kupaa na kusafiri kwenye maji kama meli.Muda mfupi baadae ilipoteza mawasiliano jambo ambalo lilileta wasiwasi miongoni mwa wahusika wa kambi hiyo ya ngome ya Lauderdale.ndani ya saa nzima,ndege nyingine zaidi zilirushwa ili kusaidia katika utafiti huo.Kwa kweli hali ya hewa ilikuwa mbaya na bahari iliripotiwa kuchafuka kwa hali ya hatari zaidi.Ndege moja tena ya Martin Mariner ( Training 49 ) ilishindwa kutoa majibu katika mawimbi ya radio.
              Muda wa saa 1:50 usiku,radio za meli moja iliyokuwa baarini zilitoa taarifa kuhusu kuonekana kwa moto mkubwa uliosababishwa na mlipuko wa ndege.Meli hiyo ilieleza kuwa baadaye palionekana kiasi kikubwa cha mafuta yakisambaa baharini na hapakupatikana mwili wowote wa majeruhi ya wa tu katika ndege hiyo iliyolipuka.Kwa kweli walishindwa kupata mafanikio yeyote kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na ya kutisha.
             Ndege hiyo ya Flight 19 kwa muda huo ilikuwa imeishiwa kabisa mafuta na ilianza kuteremka kuelekea aridhini.Mawasiliano ya mwisho na Taylor yalisikika muda wa saa1;04 za jioni.Utafutaji wa marubani hao waliopotea uliendelea usiku kucha na siku iliyofuata mamia ya ndege na meli ziliongezeka katika shughuli hiyo.
              Kwa kweli hapakupatikana rubani wowote wale.
        
             Aprili 3,1946 lilitolewa hitimisho ambalo lileta utata miongoni mwa ndugu  wa marubani waliopotea wakiwamo mama mzazi wa Taylor na mama mdogo ambao walishindwa kabisa kukubaliana na maelezo yaliyotolewa kuhusiana na tukio hilo.
             Upoteaji wa marubani hao ulileta mkanganyiko wa hali ya juu kuhusiana na Je,inawezekana vipi kwa vyombo vikubwa kama vile kuzama katika bahari fupi na kushindwa kuonekana muda wote na mahali popote pale?
             Makosa na taarifa zisizoeleweka kuhusu upoteaji wa mwanamaji na ndege ya Flight 19 muda mfupi zilianza mapema katika miaka ya hamsini.historia mbalimbali kuhusu sehemu ya kushangaza na ya kustaajabisha ambayo meli kubwa na ndogo na ndege zimepotelea hapo na "limbo of the lost" imekamata sana akili za watu kwa ghafla,gwiji lia pembe tatu ya Bermuda ilianza na bado inaendelea kuwashangaza watu mpaka leo hii.
             Taylor alikaririwa akiongea katika mawimbi ya radio akisema "Kila kitu hakiko sawa......inashangaza.....bahari haionekani kama ambavyo ilitakiwa kuwa" na "Wanaonekana kama wanatoka anga la mbali-usinitafute".Haya ni maneno ambayo yalizungumzwa na Taylor kabla ya kukata mawasiliano.Hii inapelekea kuwepo histori ya aliens katika swala la uzamishaji wa meli katika eneo la pembe tatu hilo.Hata katika move ya "Close Encounters of the Third Kind" Steven Speilberg nyaraka za Flight 19 zinakumbusha juu ya chombo kikubwa cha angani.Pia inaripotiwa kuwa katika siku ambayo upoteaji wa Flight 19 ulitokea,bahari ilikuwa tulivu.Kiukweli walikuwa wakijichanganya sana bila ya kuelewa ni nini kilitokea kwa siku ile.
             Mwaka 1991,gqzeti la habari liliandika taarifa yenye kichwa cha habari "Deep Sea" kuhusu kuonekana au kupatikana kwa mabaki ya Flight 19 katika  kina cha bahari maili kumi kaskazini mashariki kutoka katika ngome ya Lauderdale.Ndege moja yenye nambari 28,sawa na ile ya Taylor.Lakini mwezi Juni Graham Hawkes,ambaye aliongoza utafiti alisema kwamba matokeo ya utafiti wa ziada hayaoneshi kuwa mabaki yaliyopatikana hayawiani na yale ya Flight 19,hata namba za ndege hiyo hazikuwepo katika Flight 19.Pia ndege hiyo ilipata ajali muda mrefu uliopita kabla ya Flight 19 kupotea.
            Ukweli ni kwamba kumekuwa na historia mbalimbali za kustaajabisha watu kuhusu upoteaji wa meli na ndege aidha sehemu nyingine mbali na Eneo hilo la Bermuda ama ndani ya sehemu yenyewe.Ukweli ni nusu ya upoteaji  wa vyombo hivyo vya usafiri umetokea sehemu nyingine mbali kabisa na Bermuda Triangle ingawa historia inaunganishwa na eneo la Bermda,au eneo hilo la pembe tatu linaweza kuwa na nguvu ya kimaajabu inayoweza kusambaa sehemu mbalimbali za bahari na kuzizamisha meli na ndege.
            Ukweli ni kwamba ajali zinatokea kutokana na sababu moja ama nyingine,ndege zinagongana au kujigonga,meli zinazama.....hebu jaribu kuvuta kumbukumbu kwa Titanic,iliaminika kutokuweza kuzama kwa kipindi kile.Utafiti wa Larry Kusche unafafanua kuhusiana na taarifa zisizo za kweli kuhusiana na eneo lile.Baada ya kufanya utafiti bila ya kuchoka kupitia makala mbalimbali za magazeti,ripoti za hali ya hewa na nyaraka za kiofisi,Kusche alipata taarifa kama alivyohisi kwamba Bermuda Triangle haikuwa na upoteaji wowote kuliko sehemu yeyote katika dunia hii.Ana kitabu kiitwacho "The Bermuda Triangle Mystery".Tafuta ujisomee.
                    Kijana panua ubongo wako kupitia elimu.Penda kusoma katika maisha yako.