NIAJE WANA USOKITABU...
Mambo vp wana facebook,hope mko poa ile mbaya coz cjaskia vilio vya hapa na pale kwa idadi ya kutisha kama kipindi kilichopita,ila yote kwa yote nawapongeza watanzania wote kwa kusherehekea kwa amani hasa pande flani hivi za........
Kingine nawapa pole wale ambao ndugu zao hawakufanikiwa kuuona mwaka huu mpya ambao ki ukweli una dalili flani flani hivi za mafanikio,amani na kasi kubwa ya kimaendeleo.
Kingine nachotaka kuwashauri ndugu zangu,jamaa,marafiki na watanzania wote kwa ujumla ni swala la maisha.Ki ukweli kwa wale ambao ni wanafunzi wa shule za kindagate,msingi,sekondari na hata vyuo...someni jamani tena kwa nguvu zote.Siku zote penye nia pana njia na mchumia juani hulia kivulini.Hamna kitu kibaya ktk dunia hii kama kukata tamaa hasa kwa mtu ambaye damu bado changa na inachemka kama volcano kwenye CORE.Muda unaruhusu,kujikwaa sio kuanguka.Ukijikakamua hata Mungu anazidi kukupa nguvu na kukufungulia njia.Hata kwa wale wafanya biashara na shughuli mbalimbali za kimaisha,huu sio muda wa kujaribu,wenzio wanafanya kweli.Kaza buti mjomba safari i bado ndefu na vizingiti ni vingi,piga moyo konde na kaa ukitambua kua nafasi yako ipo tu hata kama unateseka na kunyanyasika kupita kiasi.
Mimi sina mengi kwa leo,ila niwatakie HERI YA MWAKA MPYA.Hakuna kama wewe na Mwenyezi Mungu kakuleta hapa Duniani kwa malengo yake binafsi.Hata wewe unaweza kufanya kama wao hakuna mtu aliyezaliwa benki au kwenye kiwanda cha pesa.Never give up...Tcchaoo!
No comments:
Post a Comment