Thursday, January 6, 2011

Baadhi ya starehe zisizo na umri maalumu.

Kweli mchezo huu ni mtamu.
       Siku zote katika maisha kuna vitu muhimu na muhimu vya kufanya.Kila mtu ana starehe yake anayo ipenda kuifanya hasa kipindi anapokuwa hana shughuli za kufanya.
Ukipita maeno mbalimbali takuta watu wakipata vinywaji kama vile vilevi,wengine hudiriki hata kutumia madawa ya kulevya ambayo ni hatari kwa afya ya akili na mwili pia.
           Vilevi kwa asilimia kubwa sio vizuri hata kidogo katika uimarishaji wa afya hata kidogo.Mara nyingi hata wataalamu wa mambo ya afya wanashauri kutotumia vilevi kupita kiasi ambapo vinaweza kupelekea hata kupoteza maisha.Vilevi hivyo ni kama utumiaji wa madawa ya kulevya ali maarufu kama NGADA,PODA,WALI NAZI,SEMBE na mengineyo kama wanavyoita vijana wa leo.
           Ki ukweli kuna starehe nyingi,muhimu na zenye kuvuti ambazo ni muhimu katika maisha ya binadamu kiafya zaidi.Starehe hizi humfanya mtu kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri,kujenga afya ya mwili na kuwa ni wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi hasa kwa ndugu zetu wana ndoa.
          Mpira wa miguu ni muhimu sana kwa afya ya mwanadamu.Mchezo huu umekuwa na umaarufu mkubwa sana katika dunia hii ambapo umegeuka kuwa ajira kwa vijana na kufanya maisha yao kuwa bora.Miongoni mwa vijana waliojijengea umaarufu hapa nchini Tanzania ni pamoja na Mrisho Ngasa,Othuman Chuji,Juma Kaseja na wengineo wengi.
          Mchezo huu umekuwa ukipendwa na watu wa rika mbalimbali wa jinsia zote mbili na ndio maana umekuwa ukijipatia umaarufu mkubwa kila kukicha.Maeneo mbalimbali yamekuwa na viwanja vya michezo ingawa unakuta havina ubora wa kutosha.Kikubwa zaidi ni serikali kuliangalia hili ili kuleta tija katika sekta hii ya michezo.Nawapongeza sana mashabiki wa soka na michezo mingine,na nnapenda kuwashauri pia vijana tujitahidi kujikita katika michezo ili kuweza kuepukana na mambo mbali mbali yasiyofaa katika jamii.Tukishindwa kuyazingatia yale mazuri tunayoambiwa na wakubwa zetu ambayo ni faida katika maisha yetu ya baadae,ki ukweli tutakua tunapotea kila kukicha.Mimi sina mengi kwa leo.

          Kauli mbiu ya leo na kesho ni "HAKUNA DUKA LENYE SPEA ZA UHAI WAKO" 

No comments: