Monday, January 10, 2011
Ngoma noma
RAHA YA NGOMA INGIA NDANI UCHEZE......
Mambo vp Watanzania wote kwa ujumla,hope mko poa ile mbaya.Ni siku mpya tena ktk safu hii ya kona ya vijana ambapo tunakuta kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii.
Leo nipo na jambo moja muhimu sana ambalo limekuwa ni kilio cha kila taifa hapa duniani hasa katika nchi zinazo endelea.UKIMWI ni tatizo ambalo ki ukweli limezua mtafaruku mkubwa sana na kuleta hofu kubwa miononi mwa wanadamu.Wanasayansi na wataalamu mbalimbali wa afya katika u;limwengu huu wamekuwa wakikosa usingizi,wakiumiza vichwa na kutumia muda mwingi sana katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili.
Serikali za kila nchi nazo zimekuwa zikitumia pesa nyingi sana katika kutoa msaada wa madawa,chakula na makazi kwa waathirika wa janga hili hasa watoto yatima.Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali wamekuwa wakiomba usiku na mchana ili kuweza kumwomba Mwenyezi Mungu aweze kutubusuru na tatizo hili.Kwa kweli ni homa ya dunia ingawa elimu inatolewa kila siku katika jamii,mashuleni,vyuoni na sehemu mbalimbali.Pamoja na viongozi,wataalamu wa afya kujitahidi kwa hali na mali kutoa elimu,bado watu hawasikii.Hii inatokana na kuwa na tamaa ya kufanya ngono isiyo salama,kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja,kuchangia vifaa vya ncha kali,kubadilisha damu isiyo salama na njia zinginezo za maambukizi.
Watu wamekuwa wakipoteza maisha,wakipoteza ndoto zao na kupoteza muelekeo katika maisha yao.Hii inatokana na watu kukata tamaa ya maisha pindi wanapojigundua kuwa wameambukizwa.Kuwa na virusi vya ukimwi si kweli kwamba utakuwa na muda mfupi sana hapa duniani! Hapana atakaye kwambia hivyo atakuwa anakudanganya.Wangapi wana maambukizi ya virusi vya ukimwi na mpaka leo bado wana ishi maisha mazuri na yenye furaha tele? Wangapi hawakuwa na maambukizi na wamepoteza maisha muda mrefu uliopia aidha kwa ajali,magonjwa mengine kama malaria? Wangapi wanazidi kupoteza maisha kwa milipuko ya mabomu katika nchi zenye vita kila siku? Jiamini na amini Mungu yupo na anasaidia.Chukua tahadhari katika maisha yako ikiwa ni pamoja na kuwalinda wale uwapendao.Kusambaza virusi sio njia ya kujikomboa au kuwakomesha watu wasio hata na makosa yoyote.Swala la kujifanya eti wewe sijui ndo mzee wa malavidavi,mzee wa totozi,shalobalo wa mtaa,bitozi nyangema,mwanaume lijali.......Angalia UKIMWI hauchagui mashalobalo wala mabitozi.Na ninyi madada zetu acheni kushawishika kirahisi rahisi,yaani ishakuwa gumzo kitaani,tuacheni kujizalilisha jamani,tusiyafananishe maisha yetu na thamani ya viepe na soda za kupita.
KIJANA JILINDE NA ILINDE NA JAMII PIA ILI TUJENGE TAIFA LA KESHO LILILO NA AFYA..SUBIRI,TUMIA CONDOM AU KUWA NA MPENZI MMOJA ALIYE MWAMINIFU.